FURAHA YA MWANAMKE

Furaha ya mwanamke imejificha kwenye mambo ambayo ni ya ajabu kidogo.

Niliwahi kusema Mahala kwamba, unatakiwa kuwa kimahusiano na mtu ambaye walau anaweza kukuletea furaha. Kama sivyo, basi aweze kuitunza furaha uliyo nayo bila kutetereshwa na makosa unayofanya.

Siku zote ukiona unakuwa na furaha pindi mtu wako anapokuwa na furaha, hayo ndiyo mapenzi.

Ukiwa unafanya haya unatakiwa kukumbuka kuwa wewe binafsi ni mhusika mkuu katika kufanya vitu vinavyokuletea furaha. Nadhani nimekuchanganya, au sio?

TWENDE KWENYE HOJA:
Tofauti na watu wanavyofikiri, mwanamke hupata furaha au hufurahishwa na mambo madogomadogo Sana ambayo pengine wanaume baadhi huyachukulia kama hayana maana au ni kupoteza muda.

Kwa mfano kwenye akaunti yangu ya Twitter kidogo watu hushangazwa na maneno yangu ambayo huwa nayaandika usiku wa manane “mpige kofi dogo matakoni(sio kumbamiza)” Watu wamekuwa wakiishia kucheka tu bila kuangalia mantiki iliyoko katika masihara haya.

Pengine watu hawajui kwamba Mwanamke unaweza kumfanyia vitu vikubwa vya gharama na bado ukaishia kuwa mtu wake wa karibu ila akaja mtu akamfungia kamba ya viatu na akawa mpenzi, mwisho wa siku akawa mume wake.

Usikose makala ijayo.

Mshambaflan

 


Elisha Nassary

History is a part of my story.

Comment

Leave A Comment

Enter your email address to subscribe to this blog and receive notifications of new posts by email.

Join 23,290 other subscribers

Copyright 2019 - Let's Write. All Rights Reserved

%d bloggers like this: