Kulipiza kisasi ni kuipa nguvu kazi ya shetani

Kisa cha punda nlihadithiwa na baba, kilikuwa hadithi tu ila sasa nmeielewa funzo

Punda alikuwa amefungwa kwenye mti. Shetani (Pepo) kwa hila akaja akaifungua ile kamba. Punde, Punda baada ya kujiona yuko huru, akaingia kwenye shamba na kuanza kula kila kitu. Mke wa mwenye Shamba (Mke wa mkulima) kuona vile, akahofia Punda anataharibu kila kitu, hivyo akachukua bunduki, akamuua yule Punda.

Mwenye Punda akaja, akaona Punda wake ameuliwa; akashikwa na hasira, akachukua bunduki yake na kumuua mke wa mkulima. Mkulima aliporudi nyumbani, na kukuta mke wake ameuliwa, akaenda kumuua Mmiliki (mwenye) wa Punda.

Watoto (wengi) wa mmiliki wa Punda kuona baba yao amaeuliwa, wakashikwa na hasira na ghadhabu, wakaenda kuchoma shamba lote la mkulima. Mkulima naye kuona hivyo, kwa hasira akawaua watoto wale wote.

Shetani alipoulizwa amefanya nini, akajibu:

– Sijafanya lolote, mi nimemfungulia Punda tu.

Umeelewa? Shetani hana nguvu ya kufanya mengi, ila machache tu ambayo yanaweza kuchokonoa na kuamsha roho ya kikatili iliyomo ndani ya mwanadamu, ya kudhuru/dhulumu/onea mwingine.

Hivyo tutafakari kabla ya kutaka kulipiza kisasi!
Kuwa mwangalifu na nafsi yako, kwa kuwa mara nyingi, Shetani ambayo hufanya ni “kufungulia tu Punda”

Leave A Comment

Enter your email address to subscribe to this blog and receive notifications of new posts by email.

Join 23,260 other subscribers

Copyright 2019 - Let's Write. All Rights Reserved

%d bloggers like this: