MAPENZI HUZALIWA NA KUFA

Kama ambavyo lugha huzaliwa na kufa kutokana na uchache wa watumiaji au sababu zingine mbalimbali, binadamu nao huzaliwa na kufa kutokana na sababu mbalimbali. Vilevile Mapenzi nayo yana uwezo wa kuzaliwa na hata kufa pia.
KUZALIWA
Dhana ya mapenzi kuzaliwa ndani ya mtu inakuja tu baada ya mtu kupata hisia chochezi za upendo na kuvutiwa na mtu wa jinsia tofauti.
Mapenzi ninayoyaongelea hapa ni ya binaadamu sio mapenzi uliyo nayo kwa Nguo za Jeans. Dhana hii imeelezewa pia na Mwandishi Idris SultanKwenye ukurasa wake wa https://www.Medium.com

Mapenzi huzaliwa kutokana na hisia za moyo ambazo huchakatwa na nafsi, na kufanyiwa maamuzi na akili, kisha mwili huyapokea maamuzi yale na kuyafanyia kazi (Response).

Hisia hizi za mapenzi huanza kwa njia mbalimbali lakini watu wasio na ulemavu kwa kiasi kikubwa hisia za mapenzi huanzia rasmi kwenye uono yaani kuona. Unakipenda unachokiona japokuwa mara nyingine unaweza kumpenda Mtu ambaye hujawahi kukutana naye wala kumwona ila huwa unamsikia labda kwenye simu au kwingine kokote. Ni kweli unaweza kujikuta unahisi kama unampenda mtu uliyemsikia bila hata kumwona lakini utakapomwona ndipo utathibitisha kile ulichokijenga moyoni mwako. Na hapo tunasema mwili umechukua hatua.

YANAKUFA
Mapenzi huishi. Ni kwa namna gani yanaishi? Mnapokuwa na ukaribu mahusiano yanakuwa ya moto na ndipo uhai wa mapenzi unathibitika. Ukaribu ninaouongelea ni ukaribu wa mawasiiano ya ana kwa ana (karibu) au hata ya mbali.
Mahusiano yaliyo hai yanahitaji mawasiliano ya mara kwa mara ili kuyaboresha na mnahitaji kuwa watu wapya ili kutochoshana.Kifo cha Mapenzi (Mahusiano) ni pale ambapo hakuna mawasiliano. Labda nikuambie tu kama una mpenzi,mna njia hai za mawasiliano,hakuna kikwazo chochote cha kiuchumi,kisiasa,kijamii kinachozuia nyie kuwasiliana ila zinapita siku 3 hamtafutani basi wewe endelea kutafta mpenzi tu maana kilichobakia ni IMETHIBITISHWA kwamba hamko pamoja tena.
HAPA TUNASEMA MAPENZI YAMEKUFA.
Hivyo basi, mapenzi huzaliwa, mapenzi hukua na mapenzi hufa pia. Ni jukumu letu kuhakikisha wapenzi wetu wako karibu kihisia wakati wote ili kuondoa kero za kuacha na kuachwa.

Life, Love, Mahusiano, Mapenzi, relationship


Elisha Nassary

History is a part of my story.

Comments (3)

Leave A Comment

Enter your email address to subscribe to this blog and receive notifications of new posts by email.

Join 22,653 other subscribers

Copyright 2019 - Let's Write. All Rights Reserved

%d bloggers like this: