Nzige wakila mazao yetu na sisi tuwale au tuwaache?

 

Kundi la Nzige lilovamia mashamba huko nchini Kenya

Kundi kubwa la Nzige lilovamia huko nchini Kenya

Taarifa ya ujio wa Nzige (Locust) katika ukanda wetu wa Afrika Mashariki zinaenea kwa kasi sana kwakweli nilivyokuwa nimesikia wanataka kuingia Tanzania jambo la kwanza lililonijia ni njaa kuingia pia, acheni masihara jamani wadudu wanakula mazao hawa.

Katika pita pita zangu mitandaoni nikakutana na takwimu zilizowekwa na tovuti ya JamiiForum namna hawa jamaa wanavyokula mazao na kumaliza kwa haraka ambapo wameandika kuwa nzige anao uwezo wa kula chakula kinachotosheleza kulisha watu 35,000 wakiwa katika kundi kubwa kama huko kwa ndugu zetu Kenya.

Waliongeza kuwa katika eneo lenye ukubwa wa kilometa za mraba 2,400 nzige wanaweza kumaliza chakula ambacho kingeliwa na watu Millioni 84 kwa siku ehee, wanakula kama raia wa Kongo kwa siku kwa mujibu wa sensa ya nchini humo wana raia wapatao Milioni 86,026,000 kwakweli na hapo kuna wale rafiki zangu wanaokula wanaacha, wengine wanamatumbo madogo unaweza kuta hawawezi vunja hii rekodi ya nzige.

Hawa nzige wanauwezo wa ‘kusepa’ na chakula cha mtu hivihivi tukabaki tunashangaa na kuanza kuulizana imekuaje mbona mahindi ghali hivi, oh kisamvu hakipatikani sokoni kumbe ni hawa jamaa wametafuna .

Nzige wamekuwa wakivamia sehemu mbalimbali toka karne na karne, vizazi na vizazi mpaka sasa limeanza kuonekana kuwa ni janga asilia hapa Afrika hasa katika ukanda wetu wa Afrika Mashariki sio kwamba halijawahi fanyiwa uchunguzi unaweza kuta kuna watu wenye wadhifa wanakesha kupambana nao lakini ndio hivyo tena.

Janga hili la nzige limenikalisha sana mitandaoni kusoma wenzetu waliowahi kupata majanga kama haya walifanyaje, si nikakutana na kisa hiki cha waarabu kwakweli kimenifurahisha sana, yaani sisi tuna kimbizana na nzige wenzetu huko wanafata ushauri wa daktari wanajenga miili yao kutokana na nzige.

Miaka ya nyuma katika Penisula ya Uarabuni ilivamiwa na nzige wakawa wanakula mazao, raia walivyoona wanamaliza kila kitu wakaamua kuweka matenga ya kutosha ya kuwatega ili wawakamate hapo ndipo wakaanza kuwatumia kama chakula kufidia uharibifu walioufanya kwenye mazao yao.

Mfanyabiashara akisubiri wateja kununua nzige huko Yemen

Waliendelea kuwala na kwakweli hakikuwadhuru kabisa bali miili yao ilijengeka vizuri tu mpaka wamama wa kiarabu wakaanza kutengeneza mbinu mpya za mapishi ya nzige wao wakawa wanaondoa kichwa,mabawa na miguu alafu wanawaanika juani mpaka wanavyokauka ndipo maufundi ya kutengeneza Roast ya nzige inaanza, nadhani ndugu zangu wahaya wamenielewa wanavyofanyaga kwa senene.

 

 

Kwa mujibu wa data za Encyclopedia ya sayansi zinasema kuwa nzige ana protini 62% na mafuta 17% hiki kiasi kizuri sana kinachohitajika mwilini hata wale wanaojaribu kufanya ‘diet’ wanaweza kuwala ili kuweka sawa mpangilio wa chakula kama wanavyofanya.

Ukiachana na maswala nilioyasema hapo juu unatakiwa ufahamu kuwa nzige ana faida lukuki mwilini kama vile;
-One of the most effective stimulants
-Treat rheumatism and back pain
-Help treat delayed growth in children
-An effective sexual stimulant especially for the elderly

Hizo ni baadhi tu ya faida zinazopatikana na hawa nzige lakini madhara yapo licha ya kwamba ni wazuri kwa kula lakini kaa ukijua wanaweza hatarisha maisha yako pia.

Hawa nzige tunao wasikia kuingia katika ukanda wetu wa Afrika Mashariki wanaitwa ‘Migratory Locust’ yaani nzige wanao hama hama, leo wapo Nakuru kesho Jinja kesho kutwa Rombo yaani hawakai sehemu moja lakini wanatabia ya kufuata mlolongo wa sehemu kutokana na mazao yalivyo.

Sasa ukisema hawa tuwaweke kwenye fungu tuuze magengeni ni mtihani hasa tutahitaji wataalamu waliangalie ili tule tupate Ma’protini’ na tunenepe lasivyo tunaweza angamia mara moja, najua unajiuliza utaangamiaje wakati umeshasikia ni kitoweo kizuri tu.

Ipo hivi, asilimia kubwa ya hawa Migratory Locust hawachagui shamba la kuvuna wao kila kitu ‘wanafyekelea mbaali’ sasa kwenye pita pita zao wanakutana na mazao ambayo yametoka kuwekewa dawa za kupambana nao na umeshasikia waarabu wanaweka matenga kuwavuna na wewe unawaiga bila kufahamu ohoo tutakukuta hospitali ndugu yangu haujielewi maana utakula sumu badala ya protini.

Sumu inayowekwa kwenye mazao ya chakula yana uwezo wa kupoteza maisha ya binadamu kwa kipindi kifupi sana kama utakosa uangalizi , kuna kisa kimoja kimeshawahi kuripotiwa kuhusu mfanyabiashara aliyeuza Kabichi kwenye msiba kwa tamaa zake alisahau kama aliweka dawa ya sumu siku kadhaa kabla ya dili kuja, akauza hivyo hivyo watu waliokula kabichi zile walipelekwa hospitali na madaktari walisema kuwa walikula chakula chenye sumu.

Usiogope sana ndugu yangu, nchini Yemen baada ya kufahamu kwamba wanaweza kula nzige wenye sumu ikaanza kampeni ya kuwafundisha namna ya kutengeneza chakula cha mifugo, lakini wanafanyaje ,wao wanawakamata kwenye matenga kama kawaida alafu wanawawatoa vichwa, miguu, mabawa kama kawaida baadae wanawaanika juani kwa kipindi cha miezi mitatu alafu baadae wanawachanganya kwenye majani ambayo yataliwa na ng’ombe , mbuzi, kondoo na wanyama wengi. Hapo mnafanya kazi ya kufurahia maziwa yenye virutubisho muhimu kutoka kwa ng’ombe.

Ukiachana na mambo niliyoyasema hapo juu kuna haja ya Mamlaka husika kulifanyia kazi swala la kupambana na hawa jamaa maana wanatishia amani, huenda hatuna utaalamu kama wa nchi za kiarabu lakini tunaweza angalia njia stahiki zitakazoweza kuwaangamiza labda tunaweza waokota tukafanya kama Yemeni.

Leave A Comment

Enter your email address to subscribe to this blog and receive notifications of new posts by email.

Join 23,260 other subscribers

Copyright 2019 - Let's Write. All Rights Reserved

%d bloggers like this: