Sayyida Salme: Binti Sultan wa Zanzibar aliyetengwa na familia kwa kuolewa na Mjerumani

Sayyida Salme alizaliwa mwaka 1844 huko Zanzibar, alikuwa ni mtoto wa 36 kati ya watoto 39, kwa aliyewahi kuwa Sultan wa Zanzibar, Sultan Seyyid Said.

Binti Sultan Sayyida Salme

Binti sultan huyu alikuwa mtundu tokea pakiwa na umri mdogo sana, moja ya matukio ya mwanzo akiwa mtoto ni kujaribu kuchukua kisu na kumchanja ngamia shingoni na alivyokamatwa aliwaambia walinzi kuwa anajifunza kuandika kiarabu jambo ambalo lilikuwa haliruhusiwi kwa mtoto wa kike kujifunza kwa kipindi hicho.
Kaka yake na Sayyida Salme, Majid ndiye aliyekuwa amerithi nafasi ya baba yake baada ya kufariki mwaka 1856, lakini kulikuwa na mfukuto wa vita ndani ya familia hiyo ya kisultani ambapo mdogo wao ajulikanae kama Bargash alitaka cheo cha kaka yake.

Kutokana na vita hiyo ya familia Binti Sultani aliamua kumuunga mkono kaka yake Bargash akiwa na miaka 15 alifikia hatua ya kuwaandikia barua baadhi ya machifu kumuunga mkono kaka yake huyo ili awe Sultan wa Zanzibar na Oman. Lakini yote aliyoyafanya hayakuweza kuzaa matunda kwani kaka yake Bargash aliweza kutiwa nguvuni na kaka yao mkubwa Sultan Majid na hapo Binti Sultan Salme aliamua kumwangukia kaka yake lakini kuanzia hapo ndugu zake 36 walikuwa hawashirikiani naye kwa jambo lolote lile kumhuusu.

Sayyida Salme akiwa na familia yake, watoto wake watatu na Mume wake Rudolph Ruete

Baada ya kuwa mpweke kwa muda mrefu kutokana na kutengwa na ndugu zake na kujiona kama mkimbizi ndani ya familia , Binti Sultan Salme aliamua kuhamia karibu na mtaa wa Stone Town ambako alikuwa jirani na mfanyabiashara wa kijerumani aitwaye,Rudolph Heinrich Ruete ‘ambaye baadae alikuwa baba watoto wake’

Wafanyabiashara wengi wa kigeni walikuwa wakimuona kama anawazibia riski katika biashara zake anawafanya wasifanya biashara zao na kuishi kwa amani katika eneo hilo wakihofia kufwata na walinzi kutoka katika kasri ya kisultani kumuangalia binti sultan Salme.

Binti Sultan Salme hakujali yote waliokuwa wanafikiria hawa wafanyabiashara wa Kijerumani yeye alitaka kuishi kwa amani na sio jambo jingine.Sasa hapo ndipo akaanza mahusiano ya kisiri na jirani yake Rudolph Ruete mjerumani.

Licha ya kwamba mahusiano yao yalikuwa ya siri lakini walionekana siku moja na kiongozi wa wafanyabiashara wa eneo hilo ambaye aliona kuwa iwapo Sultan Majid kaka wa Salme akijakujua watafukuzwa kwahiyo akaamua kupenyesha umbea kwa baadhi ya Maaskari waaminifu wa Sultan ndio wakaanza kumpenyezea taarifa taarifa za Dada yake, Sultan Majid akatoa amri ya kuchunguzwa kwa ndugu yake kama kweli anatoka kimahusiano na Mjerumani taarifa ilipelekwa kwake kuwa ni uvumi tu.

Miezi kadhaa ilipita bila ya uthibitisho wowote kuwa Binti Sultan anatoka kimapenzi na mfanyabiashara wa kijerumani mpaka paka pale msemo wa Mimba haifichiki ulivyothibitika kwa binti huyu wa kisultan ambapo mimba yake ilianza kuonekana na ndipo hapo walinzi walimpa taarifa Sultan Majjid alisikitika sana akaona ili aondokane na aibu hiyo ya mdogo wake akaamuru wampeleke Saudi Arabia.

Sayyida alikuwa binti mwerevu sana alishawahi sikia baadhi ya hadithi zinazoendana na majanga yake ambao wengi wao walivyopelekwa uhamishoni walijitahidi kutoroka sasa nayeye akawa na mpango huo huo ikabidi ampange jamaa wake mjerumani wakutane Yemeni.

Safari ya Binti Sultan Sayyida kwenda uhamishoni akiwa safarini wakati Jahazi yao ilivyokuwa imepumzika katika bandari ya Yemen katika mji wa ADEN, hapo ndipo akachukua maamuzi ya kutoroka, mpango wake ulifanikiwa kwa asilimia mia (100%).

Akiwa nchini Yemen akafanikiwa kujifungua lakini motto alifariki hakukaa hata mwezi, kuna watu wanadai kuwa walikaa masheikh Zanzibar ili kuondoa kizazi cha kizungu katika familia hiyo kwa kumpoteza mtoto wa Sayyida.

Miezi michache baadae Binti Sultan aliungana na mpenzi wake Ruete ambapo baadae walioana na kuhamia nchini Ujerumani, akabadilisha dini kuwa mkristo jina lake jipya likawa Emily Ruete na sio tena Sayyida Salme, wakafanikiwa pia kupata watoto watatu.

Muda mfupi baada ya Salme kupata mtoto wa tatu mume wake Rudolph Ruette alipata ajali ya kugongwa na treni za mjini Ujerumani (Tram Accident) na kufariki hapo hapo.

Ulikuwa wakati mgumu sana kwa Sayyida Salme kuliko vipindi vyote alivyowahi pitia katika maisha yake alijiona hafai katika jamii akiwa ameachwa na watoto wake watatu. Mambo yote haya yalimfanya afikirie kuandika kitabu kinachohusu maisha yake na mazuri, magumu, panda na shuka aielezee Dunia yote lakini hakufanya hivyo zaidi aliacha picha pamoja na panga la kisultani la baba yake.

Salme alifariki Dunia mwaka 1924 ambapo alizikwa pamoja na kikapu chake alichokuwa anakipenda sana ambacho alipewa zawadi na mama yake akiwa Zanzibar.

 

Leave A Comment

Enter your email address to subscribe to this blog and receive notifications of new posts by email.

Join 23,260 other subscribers

Copyright 2019 - Let's Write. All Rights Reserved

%d bloggers like this: