Sio bora kazi, ila kazi bora

Kumekucha kichele. Ningali nagaagaa. Japo mda wasonga, nina azma kuinuka  ila nahisi siwezi. Naelewa fika mahukumu yangu kazini. Naelewa zaidi wajibu wangu kuhitajia kujizatiti kutarazaki. Sijasahau katu, bila juhudi mjini utapaona pachungu. Kipi kinacho nikwaza kikanitia zohali hata nisinyanyuke?

Hili swala sikulipa umuhimu kwa mda. Hata nilipo pata ushauri nasaha na kujitathmini. Tatizo hili lawasibu wengi. Yote yatokana na shughuli usioipenda. Ndivyo alivyonishauri mtaalam. Hicho ni kiashiria tu. Msongo wa mawazo na hata kuumwa. Kufanya kazi kama roboti bila kuijali wala kuwa ma mapenzi nayo. Mja anae hisi kukwazwa na kukifanya asichokipenda bora kubadili mbinu na kuanza mchakato wa kusaka shughuli mbadala. Kazi mbadala. Ilimradi moyo wako wairidhia. Katika mkono kwenda kinywani, Sio bora kazi tu. Bali kazi bora. Kufanya ukipendacho

Leave A Comment

Enter your email address to subscribe to this blog and receive notifications of new posts by email.

Join 22,025 other subscribers

Copyright 2019 - Let's Write. All Rights Reserved

%d bloggers like this: