Tumia Busara na Hekima

HEKIMA YA KIPOFU:

Sikumoja, mida ya jioni, jua kukutwa, kipofu alitoka kwenda mtoni ili anywe maji. Alikuwa mkononi mwake ameshika taa kwa ajili ya kumuangazia njia.

Mmoja katika wenye kuona akamuuliza kipofu: kwanini unabeba taa hali haikunufaishi kwa chochote?

Kipofu akamjibu: Naibeba ili wenye kuona wasije kunigonga au kunipamia.

Hekima ni kama mbeba taa nae ni kipofu. Unawapa faida wengine na lakini faida hio ni kwa manufaa yako mwenyewe.

Hili likanikumbusha neno katika andiko la kiislamu

*{وَمَن يُؤۡتَ ٱلۡحِكۡمَةَ فَقَدۡ أُوتِيَ خَيۡرٗا كَثِيرٗاۗ}*
Na aliye pewa hekima bila ya shaka amepewa kheri nyingi.

Mwandishi : Yussuf Mwinyi

 

Leave A Comment

Enter your email address to subscribe to this blog and receive notifications of new posts by email.

Join 23,432 other subscribers

Copyright 2019 - Let's Write. All Rights Reserved

%d bloggers like this: