TUWALINDE WALE TUWAPENDAO

 

Habari zenu mabibi na mabwana. Nimeona Kiswahili kinanifaa zaidi kuwasilisha ujumbe huu. Ahsante kwa kujiunga nami! Twende sambamba!

Nadhani mbali na chuki, sote tuna watu ambao tunawapenda. Hawa yawezekana ni mpenzi, mke, mume familia au ndugu wengine.Tunalo  jukumu kubwa la kuhakikisha kwamba tunailinda furaha ya wale tuwapendao. Hiki hapa ni kisa kifupi kuhusu namna mwanaume huyu alivyohakikisha mke wake ana haki na hazina ya furaha aliyokuwa nayo hapo kabla na hata baadaye.

∗∗∗∗∗∗∗

Kabla ya kuondoka kwenda kazini nilimwachia mke wangu Tsh 10000 (noti mbili za elfu tano) ikiwa ndicho kiasi pekee nilicho nacho mfukoni na ndani kiujumla.
Mke wangu alienda gengeni kufanya manunuzi ili tupate chochote kitu. Akiwa anatoa hela aligundua kumbe noti ya pili haipo mifukoni mwake, imepotea. Alirudi nyumbani kwa unyonge na nilipomwuliza tatizo alifululiza kulia tu. Nilitoka kidogo nikaongea na mdogo wangu aniazime Tsh 5000 na akanipatia mkononi. Nilirudi ndani na kuidondosha ile elfu 5 koridoni mwa nyumba yetu. Wakati huo Niliendelea kumbeleza mke wangu ili asizidi kusomeka maana hali yangu kwa wakati huo aliielewa kuwa ni ngumu hivyo kupoteza kiasi kile cha hela ingekuwa “kitenzi kichokozi cha umaskini”. Muda wa kwenda kazini ulipofika nikaaga na kwenda kazini huku nikimsisitiza azidi kuitafuta ile hela kwa makini na utulivu mkubwa maana siamini kama imepotea kabisa kisha nikaondoka zangu “by Ngondi” huku nadunda ndogondogo kutokuonyesha uso wangu wenye masononeko na umaskini ndani yake.
Nikiwa kazini simu yangu iliita. Hapo nikaisikia sauti nyororo iliyojawa mahaba na isiyojua kuchepuka ni nini, sauti ya mke  wangu kipenzi akiongea kwa furaha na kusema “mme wangu ile hela nimeipata” japo ni kwenye simu lakini nafikiri aliliona tabasamu langu na uso wangu ule usiokuwa na kunyanzi hata moja la mkopo huku nikimsifia. Kumbe nina langu moyoni. Hela hajaipata wala nini! Nimeitega mimi mwenyewe.

Wapendwa, Tuilinde furaha ya wale tuwapendao kwa gharama yoyote. Hazina ya furaha waliyo nayo haitakiwi kupotea kizembe. Hatupaswi kuyaruhusu maumivu yatese mioyo yao wasije kutuambukiza nasi tukaumia.

“If her happiness makes you happy, that’s called LOVE”

Mshambaflan

Life, Love, Mahusiano, Mapenzi


Elisha Nassary

History is a part of my story.

Comments (2)

Leave A Comment

Enter your email address to subscribe to this blog and receive notifications of new posts by email.

Join 23,260 other subscribers

Copyright 2019 - Let's Write. All Rights Reserved

%d bloggers like this: