TWITTER WAMESHINDWA KUDHIBITI NGONO?


Twitter ni mojawapo kati ya mitandao mitatu maarufu ya kijamii Instagram,Facebook&Twitter yenye watumiaji hai zaidi ya 139M kwa siku ikiwa ni makadirio ya ongezeko la 14% mwaka hadi mwaka. Utumiaji huu ukiwaingizia zaidi ya Mabilioni kwa mujibu wa https://adweek.it/2yglyQG

★ Twitter ikoje hasa?

Twitter ni mtandao uliojikita zaidi katika kutoa habari mpasuko kuhusu siasa,michezo,burudani,muziki,fasheni na Habari zingine mbalimbali. Hivyo hata watumiaji waliothibitishwa (Verified users) hutokana na nyanja hizo.

• Twitter imekuwa na mwenendo mzuri tangu mwaka 2006 ilipoanzishwa rasmi. Imekuwa ikisimamia misingi na makubaliano ya matumizi baina yao na watumiaji wake (User Agreement Policy) hivyo anayekwenda kinyume na makubaliano huchukuliwa hatua. Mojawapo ya hatua hizo ni pamoja na akaunti kusitishwa.

• Mitandao mingine ya kijamii hasa Instagram imekuwa kinara katika kusimamia sheria za matumizi hasa katika kipengele cha udhalilishaji (Cyber Bullying) pamoja na uhalifu mwingine.

•Ni kazi ngumu sana na pengine ukiingia sasahivi Instagram ukaenda sehemu ya “Tafuta” huwezi kuona akaunti yenye video za ngono au picha za uchi wazi.

• Vilevile Instagram ukiweka video ya wimbo wa msanii bila idhini yake itazuiliwa ndani ya dakika kadhaa tu kutokana na sheria za matumizi zisizoruhusu wizi wa maudhui.

Sasa hamia upande wa Twitter uone maajabu:

Akaunti za Twitter zinazoweka video za ngono zipo zaidi ya maelfu. Nenda Twitter sehemu ya “Tafuta” kisha jaribu kuandika yahusuyo ‘porn’ ujionee palivyojaa uozo.

• Kuna akaunti za Twitter zina zaidi ya miaka miwili,zina wafuasi zaidi ya 200K na zinarusha video za ngono kila baada ya saa au dakika ila hazijasitishwa.

Sawa, pengine yawezekana ndizo zinazoongeza idadi ya watumiaji na kukuza biashara zao kila uchwao hadi kuingiza Bilioni 400,lakini ni sahihi? Sheria za matumizi za Twitter haziruhusu mambo haya lakini uchukuaji hatua umekuwa wa kusitasita. Kila kukicha tunapoteza idadi ya watu wenye nguvu kutokana na punyeto zinazochangiwa na video ziwekwazo Twitter(madaktari watasema).

• Wanaoangalia video za ngono Twitter ni mamilioni ya watu kwa siku. Sio rahisi kugundua bila kuingia kwenye eneo la “search” kwa wale ambao hawajafuta. Wengi huingia Twitter kwa lengo la kuangalia ngono na wanahamasishwa na maudhui haya hafifu yanayoruhusiwa na Twitter.

• Ifike mahala Twitter wawe na mchakato wa data za matumizi wa haraka ili kudhibiti matumizi yasiyofaa ya mtandao huu pendwa kama wafanyavyo Instagram. Asanteni!

NASSARY A Writer,Author and a Poet in making

Twitter


Elisha Nassary

History is a part of my story.

Leave A Comment

Enter your email address to subscribe to this blog and receive notifications of new posts by email.

Join 23,260 other subscribers

Copyright 2019 - Let's Write. All Rights Reserved

%d bloggers like this: