UNADHANI PICHA NI MUHIMU?

Unadhani Picha ni Muhimu?

Ndio, Katika ulimwengu wa sasa ni kitu cha kawaida sana kukumbana na picha za watu mbalimbali kwenye mitandao ya Kijamii. Zipo picha za watu wa kawaida na picha za watu maarufu. Watu maarufu huweka picha kwenye mitandao ya kijamii kama Instagram, Twitter, Facebook ili kushikilia ile hadhi waliyo nayo, kutangaza biashara pamoja na kuhamasisha mambo fulani katika jamii.

JE! KUNA UMUHIMU WA KUWEKA PICHA ZETU MITANDAONI?

Kwa mtazamo wa kawaida, Picha ni muhimu sana katika kutukumbusha nyakati mbalimbali tunazopitia maishani mwetu; nyakati za furaha, nyakati za karaha, vilevile picha ni utambulisho. Hututambulisha kwa umma kwamba sisi ni watu gani na tunafanya nini.

MTAZAMO

Mpaka kufikia mwaka 2017, bado niliamini katika kuweka picha zangu mitandaoni. Hii nilitumia kama njia ya kujifurahisha tu. Ndio maana unaweza kutembelea mtandao wa Facebook sasahivi ukakuta watu zaidi ya 100 mnaofahamiana wameweka picha zao huko, huku wakiziambatanisha na maneno mafupi ambayo pengine hata hayana uhusiano na picha yenyewe. Mfano mtu ameweka picha na kuandika “Baby I am so scared, naogopa kuingia mwaka mpya 2020” akaunganisha na baadhi ya emoji ambazo hajui maana yake 😂🤗.

Turudi kwenye mada. Mawazo yangu ya uwekaji picha kiholela kwenye mitandao ya kijamii yalikuja kubadilika baada ya kuona udhalilishaji wanaofanyiwa watu baadhi kupitia utambulisho wao (Picha) kwasababu tu ya kutofautiana kimtazamo. Kuna wanawake wamenyanyaswa kupitia picha zao, kuna wanawake ambao picha zao sasahivi zinatumika kufanyia utapeli mitandaoni. Mfano mzuri ni Instagram, Twitter na Facebook. Watumiaji ambao wamekuwa wakiathirika sana ni wanaume wenye tamaa au wafanyao mambo kwa mihemko. Watu wametuma sana nauli kwa wanaume wenzao wakidhania ni wanawake warembo kutokana na matumizi ya picha. Kwa maana hiyo hata wanaume wamenyanyasika sana. Sababu ya haya yote ni picha za mitandaoni. Ndio maana nikauliza Je! Unadhani Picha ni muhimu?

MTAZAMO

Nilikuja kuona mitandao ni sehemu salama pia hata kama hutoweka picha zako. Ndio maana mwaka 2017 nikafuta picha zangu zote kwenye mitandao ya kijamii na kuzihifadhi sehemu salama kwa matumizi mengine. Najua kwamba kuna ulazima wa kuweka picha pale ambapo unakuwa na shughuli maalum kama vile picha za matukio, picha za uhamasishaji au hata matangazo. Kama hakuna ulazima wa kuweka picha yako basi nikushauri usiweke ili tu kuwafurahisha watu au upate Likes. Utakuwa na utambulisho mwingine ambao ni Jina, kazi na hata maneno yanaweza kukutambulisha pia.

UNATAKA KUHIFADHI PICHA?

Wengine wanaweza kusema wanaweka picha mitandaoni kwa kumbukizi za baadaye. Ni kweli, lakini kuna njia mbalimbali za kidigitali za utunzaji mafaili. Mfano Google Drive, Google photos na kadhalika. Hizi unafanya kuziunganisha na simu yako tu. Kwa maelezo zaidi juu ya hili tembelea www.Twitter.com/SimuYako

HITIMISHO

Ndugu msomaji, nia yangu ya kukueleza haya yote sio kukuonyesha kwamba wewe uwekaye picha mitandoni ni Punguani, La! hasha. Ni tahadhari tu kutokana na hasara nyingi zitokanazo na jambo hili kuliko faida zake. Shuhuda ni nyingi sana siwezi kuziweka hapa.

Kama utapenda kuweka picha mitandaoni uwe tayari kwa athari hasi na chanya. Picha zisiwe chanzo cha mfadhaiko, Mkazo na msongo wa mawazo.

Mwisho!

Unaweza kusoma makala nyingine zilizopita kwa kubofya hapa Ninacho cha kusimulia Au mapenzi huzaliwa na kufa

mitandao, Picha


Elisha Nassary

History is a part of my story.

Leave A Comment

Enter your email address to subscribe to this blog and receive notifications of new posts by email.

Join 23,290 other subscribers

Copyright 2019 - Let's Write. All Rights Reserved

%d bloggers like this: