Upweke ni uvundo ila kaa pweke usalimike

Maajabu ya mwanaadamu ni kuwahitajia wenziwe kiasi ya kutoweza kuishi pweke. Japo mahitaji yote atayapata ni muhali kuukubali upweke, wavyele wakauita uvundo. Walioisoma saikolojia wakabaini adahabu iliokuwa yakutesa zaidi nikumtenga na jamii kwa aliehukumiwa.

Ila katika kuamiliana na wenziwe, waja hawaliwezi bila sheria na dini. Mikwaruzano baina yao ni mingi mno na kusutana, kejeli na masengenyo. Baada ya yote tutagundua hitaji yetu kwa wenzetu ni masilahi tu. Na ndio chanzo cha kujijengea ua za kuta ndefu na wenye uwezo kuhamia nje ya mji. Wasifu mkubwa wa kunadi makaazi mapya siku hizi ni kuwa ‘ eneo tulivu isiokuwa na muingiliano na watu’ kila mmoja na ua iliomzunguka kimombo “gated  area/ community”

Ishi kwa wema na watu, ila dumisha mipaka. Kumbuka fadhila mfadhili mbuzi  mwanadamu ana mauzi (maudhi). Ni kweli ushairi wa marehemu  baba mtaka nyingi nasaba, hupata nyingi misiba.

Comment

  • Inda na wivu,huleta chokochoko.Usahaufu,utofauti wa mapato kikawa kigezo Cha vipimo baina ya jamii,ndugu na hata marafiki. Ikawa binadamu kujiweka mafungu,huku hautoshi huku watoshea ama ukakosa vyote kukusukuma kuwa pweke.Hali hii ni ngumu na huhitati nasaha njema ya kiakili na mawazo. Hivi basi wanahesabika wenye uwezo wakukaa pweke bila udhuru

Leave A Comment

Enter your email address to subscribe to this blog and receive notifications of new posts by email.

Join 21,962 other subscribers

Copyright 2019 - Let's Write. All Rights Reserved

%d bloggers like this: