USHINDI WA UTULIVU

Magazeti yote ,mitandao ya kijamii na vyombo vya habari vilikua vikieleza kituko cha mwaka ambacho Donlia alikifanya.Pamoja na kwamba hakukua na ushahidi kuwa ni kweli yeye ndio aliyefanya,lakini kwa namna vyombo vya habari vilivyojitutumua kueleza habari hii,hakuna aliyesalia kutoamini ukweli huo.Katika meza yake yalikuwako magazeti saba na yote yalijaa vichwa vya habari vilivyolipandisha joto la mwili wake.Machozi aliyolia asubuhi ile yalitosha kukausha sebule ile ya kipenyo mita cha 7.8,macho yalivimba na machozi hayakutoka tena.
Akaunti zake zote za mitandao ya kijamii zilikua na malaki ya wafuasi na kuthibitishwa kwa ‘blue tick’.Hivyo jumbe zilimiminika mithili ya mvua za El-nino,kwa ujasiri mkubwa aliichukua ile simu na kuivunja,kisha akabeba yale magazeti na kuyachoma yote moto.Moyoni akanuia kuanza maisha mapya.

Donlia Zelp ,binti aliyesifika kwa umahiri wa sanaa ya kuelimisha jamii hasa katika kipindi chake cha mubashara runingani kilichoitwa ‘DoZe panorama’.Hakuwa mtu wa makuu,alipendwa na jamii nzima,hakuacha kupokea jumbe za pongezi kila mara,alipokea tuzo zisizopungua tatu kila mwaka.Lakini hayo yote yalihitimishwa kwa taarifa moja tu yakubuniwa isiyokua sahihi.Ilichukua sana muda kwa Donnlia kuwa sawa,lakini kama walivyokua wanadamu haikuchukua miezi miwili kila kitu kilisahaulika.Japo Donlia alipoteza kabisa umaarufu wake na hakuweza tena kuendesha vipindi vyake vya kuelimisha jamii.

Zipo namna nyingi tofauti ambazo watu maarufu hupoteza nafasi zao hasa pale wakati wao unapoisha.Wengine hupotea tu,wengine hupotezwa na wengine muda wao unakua umewapita.Ni vyema sana kila mtu akajua nafasi aliyonayo sasa ipo siku hatokua nayo tena,na nafasi hizo zitachukuliwa na watu wengine,hata kama sio nafasi ya kuwa mtu maarufu lakini nafasi iliyopo kwako kuna wakati haitokua yako.
Wanamageuzi hawapambani kupata nafasi walizonazo,hupambana kupata nafasi wasiokua nazo.Kila kinachosikika leo kwa mvumo,kuna wakati kilikua kimetulia kimya.Na sifa mojawapo ya ushindi ni utulivu.Wengi hatuwezi kudumu katika nafasi tulizopo kwa sababu tumesahau kanuni hii.Kuna watu tunaweza kusema viwango vyao vya ubora havijawahi kushuka kwasababu wamepata ushindi wa utulivu.Watu waliofanya mapinduzi walitumia kanuni hii ya ushindi wa utulivu na kuhakikisha wamepata nafasi zisizokua zao,na pale waliposahau kanuni hii hawakubaki salama,nao walipinduliwa.
Washindi wa utulivu hukubali kushushwa vigezo na pengine kudharaulika lakini hawakukubali kupoteza walichokua nacho ndani.Hukubali kulipoteza vazi lao la nje ili kukilinda kilicho ndani yao.

USHINDI WA UTULIVU NI KUTOKUSHUKA VIWANGO VYA UBORA WAKATI WOTE.

Comments (4)

Leave A Comment

Enter your email address to subscribe to this blog and receive notifications of new posts by email.

Join 22,653 other subscribers

Copyright 2019 - Let's Write. All Rights Reserved

%d bloggers like this: