WASIWASI AKILI

 

Asilimia kubwa ya walio wengi tumekua tukiamini kuwa walioshinda wengi na waliofanikiwa walikua majasiri katika kukabiliana na hali zao.Sipingani na dhana hii ambayo ukweli wake umekua ukidhihirika kila leo,lakini jambo moja tu ambalo utakua hujalitambua ni kuwa “Majasiri ni washindi wa sasa,lakini wenye hofu ni washindi wa baadae” hivyo hilo ni suala la muda tu.

Viongozi wengi ambao walitawala nchi zao kwa mkono wa chuma na waliobakiza hazina zao duniani ziitwazo udikteta, tena wanaosadikika kuwa walikua majasiri kupita kiasi,ndio walioongoza kuwa na wasiwasi na hofu.Hakuna dikteta aliyeishi bila wasiwasi wa kufurushwa madarakani wala hofu ya kupinduliwa.Hali hii ya kuwa na hofu na wasiwasi ndio iliyowafanya wayamudu madaraka dhalimu waliyoyapokea kutoka kwenye mikono ya damu na machozi ya wazalendo.

Ninakumbuka kisa cha “operesheni Entebbe”,ambapo waisraeli walipanga namna ya kuwanusuru mateka wa kiisraeli waliokua wameshikiliwa katika uwanja wa ndege wa Entebbe na nduli Iddi Amini.Katika mpango huo waokoaji hao walipanga kutumia muundo wa msafara kama ule aliotumia Iddi Amini wakati alipokua akizuru uwanjani hapo kuwasalimu mateka.Iddi Amini alipenda kutumia gari yake ndogo nyeusi na ikifuatiwa na gari ya wanajeshi waliomlinda,hivyo baada ya waokoaji hao kuusoma msafara wake,walijaribu kuiga kila ilivyo ili kuufanana.Walipenyeza na hadi kujua siku gani Iddi Amin hatokuepo nchini,na walifanikiwa kujua.Iddi Amini alikua akielekea katika mkutano wa AU(African Union),na ndipo walipotumia wasaa huu vilivyo.Basi wale waokoaji wakiisraeli waliingia pale uwanjani mithili ya msafara wa Iddi Amini,lakini katika hali isiyokua ya kawaida walistaajabu pale waliponyooshewa silaha hata kabla hawajaingia uwanjani.Siku moja kabla Iddi Amini hajaondoka nchini alibadili rangi ya gari yake kutoka nyeusi na kuwa nyeupe,jambo ambalo lilitokana na wasiwasi aliokua nao.Na hiyo ilipelekea wale waokoaji wa kiisraeli kushtukiwa mapema(japo walifanikiwa katika mpango wao wa kuwakomboa mateka wao).

Katika kipindi tulichopo,watu wenye wasiwasi,woga na hofu wamekua wakichukuliwa kama ni watu dhaifu.Wamekua wakichukuliwa kama hawawezi kuhimili mikiki mikiki ya maisha.Kama ambavyo zimekuwapo njia mbili tu za kumshinda simba;yaani kuwa jasiri na kumkabili au kuogopa na kutimua mbio,ndivyo njia hizo hutumika pia katika kupambana na hali ngumu.

Kuwa na wasiwasi juu ya jambo kunaweza kukufanya ukalishinda na pia kuwa na hofu au woga ndio njia pekee ya kushinda jambo lililo nje ya uwezo wako.Sio kila jambo ni la kupambana,mengine yanahitaji hofu tu au wasiwasi tu na ndio basi yanakuwa yameyeyuka kama barafu ya kiangazi.
Usijisikie dhaifu kuitwa mwoga,japo sio kwamba woga utakusaidia katika kila nyanja lakini hofu na wasiwasi ni nguzo muhimu za mshindi.
WASIWASI AKILI,HOFU NI ULINZI

Comment

Leave A Comment

Enter your email address to subscribe to this blog and receive notifications of new posts by email.

Join 23,260 other subscribers

Copyright 2019 - Let's Write. All Rights Reserved

%d bloggers like this: